Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa Magereza Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo Jumanne, Februari 10, 2025 kwenye dimba la Sokoine, Mbeya.

Mabao ya Coastal Union yalifungwa na Bakari Msimu dakika ya 1, 51, Shiza Kichuya dakika  ya 42, na  Cleopache Mkandala dakika ya 90+, huku bao la kufutia machozi  la Prisons likifungwa na  George Mpole dakika ya 45.

Kwa matokeo  hali bado ni mbaya kwa Tanzania Prisons iliyopo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tisa. Kwa upande wao, Coastal Union imefikisha pointi 14, ikipanda hadi nafasi ya tisa kutoka nafasi ya 13.

Kocha Msaidizi wa Prisons, Innocent Mwamgonde amesema waliingia uwanjani kwa lengo la kushinda mechi lakini umakini wa wachezaji haukuwa mzuri na  wapinzani wao walifanikiwa kutumia makosa waliyofanya na kupata ushindi.

Naye Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mohammed Muya amesema ushindi huo ni zawadi ya  uvumilivu wa viongozi na mashabiki wao kwani walipitia kipindi kigumu  cha kukosa matokeo mazuri.

Pamba yatakata Mwanza

Katika mchezo mwingine, Pamba Jiji imeibuka na  ushindi nyumbani wa bao 1-0 dhidi Namungo  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Bao hilo likifungwa na Methew Momanyi dakika ya 53.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...

Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic...

IAEA yaipongeza Zanzibar kwa Ushirikiano Katika Kilimo na Mifugo

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Suleiman Masoud Makame,...

More like this