Mwili wa Jenista Mhagama Kuzikwa Jumanne Mbinga, Ruvuma

Na Mwandishi Wetu

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya Disemba 16, 2025 katika Kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma.

Mhagama ambaye amekuwa Mbunge wa Peramiho kuanzia mwaka 2005, amefariki dunia jana Alhamisi, Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.

Ratiba ya mazishi yake iliyotolewa usiku wa Alhamisi na uongozi wa Bunge, inaonesha Ijumaa, mwili wake utapelekwa nyumbani kwake Itega, jijini Dodoma.

Jumamosi ya Disemba 13, 2025, mwili wa Jenista utapelekwa Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege itakapofanyika ibada.

Viongozi mbalimbali watahudhuria kanisani hapo wakiwemo Spika wa Bunge, Mussa Zungu, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba na Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baada ya shughuli ya hapo kanisani, mwili wa Jenista utasafirishwa kwenda Songea, Mkoa wa Ruvuma.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

SAMIA AONGOZA TAIFA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOA KWA AJILI YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wananchi, viongozi wa Serikali na wakuu wa vyombo vya...

e-GA YASIFU MAGEUZI YA TANESCO KATIKA UTOAJI HUDUMA KIDIGITALI

📌 Wavutiwa namna TANESCO inavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutoa huduma nzuri kwa...

KAIMU MSAJILI TPRB ASHIRIKI MAFUNZO ELEKEZI YA UONGOZI KWA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI, MASHIRIKA YA UMMA NA WAKALA ZA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB),...

More like this