Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria za nchi na kuepuka kuingilia au kushiriki katika vitendo vyovyote vinavyoweza kuathiri au kuingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025 wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uangalizi.

Wito huo umetolewa leo tarehe 17 Oktoba 2025 na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, wakati akifungua kikao cha siku moja na Waangalizi hao kwa lengo la kuwapa maelekezo, taarifa muhimu na miongozo kuhusu namna ya kutekeleza majukumu yao ya uangalizi wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Katika hotuba yake, Jaji Asina amewakumbusha waangalizi hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uhuru, na kutokuwa na upendeleo, huku wakizingatia sheria za nchi na Mwongozo wa Waangalizi wa Uchaguzi wa mwaka 2025.

“Waangalizi wanapaswa kuepuka kuingilia shughuli za uchaguzi, kutoonyesha dhihaka kwa watendaji wa uchaguzi, au kutoa maelekezo kwa maafisa wa Tume kuhusu namna ya kufanya kazi zao,” amesisitiza Jaji Asina.

Jaji Asina ameongeza kuwa endapo kuna malalamiko au dosari yoyote inayojitokeza, waangalizi hao hawana budi kuwasilisha malalamiko hayo kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa njia ya Tume.

Katika kikao hicho, mada tatu kuu ziliwasilishwa kwa waangalizi wa uchaguzi ambapo mada ya Maandalizi ya Uchaguzi iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi mada ya ma Masuala ya Usalama iliwasilishwa na mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, na mada kuhusu Masuala ya Afya iliwasilishwa na mwakilishi kutoka Wizara ya Afya.

Pia Waangalizi hao walikabidhiwa nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

Nyaraka hizo ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya 2024, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya 2024, Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2025, Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa 2025 na Mwongozo wa Waangalizi wa Uchaguzi wa 2025.

Aidha, walikabidhiwa vitambulisho rasmi na kuaswa kuvitumia wakati wote wa kutekeleza majukumu yao.

Pia walihimizwa kujitambulisha kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika maeneo watakayofika ili kurahisisha ushirikiano na kupata msaada inapohitajika.

spot_img

Latest articles

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

More like this

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...