Askofu Malasusa: Prof. Mmari alikuwa mnyenyekevu, mcha Mungu

Na Winfrida Mtoi

Mkuu wa Kanisa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa ameongoza Ibada ya kuaga mwili wa Prof. Geoffrey Mmari, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Tumaini Dar es Salaam University College (TUDARco) ambacho sasa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tumaini (DarTU),

 Ibada hiyo imefanyika leo Oktoba 14,2026 katika Kanisa Kuu Azania Front jijini Dar es Salaam, huku waombolezaji walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho.

Akizunguza wakati wa ibada hiyo, Askofu Malasusa, amemtaja marehemu Prof. Mmari kuwa ni mtu aliyelelewa katika misingi ya unyenyekefu na baba yake aliyekuwa mchungaji na ameendelea kufundisha hadi watoto wake.

“Mimi nina uhakika kwa sababu naifahamu familia ya Prof. Geoffrey Mmari, ni wanyenyekevu kwa sababu walifundishwa sio tu kwa Geoffrey Mmari, tangu babu ameendelea kufundisha. Niwaombe wazazi tuendelee kufundisha watoto wetu,” amesema Askofu Malasusa.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tumaini (DarTU), Prof. Burton Mwamila amesema Prof. Mmari aliweka misingi imara ya kitaasisi, iliyochangia kufanikisha maendeleo ya chuo hicho na kukiwezesha kupanda hadhi kuwa chuo kikuu kamili mwaka 2024 a kupewa jina jipya la DarTU.

 Askofu Mstaafu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Kati, Prof. Hance Mwakabana amesema katika Prof. Mmari  alikuwa mwalimu  wao mzuri na alimheshimu kila mwanafunzi wake na aliwapenda na  ilikuwa ngumu kumkosea.

 Marehemu Prof. Mmari alifariki mchana wa Oktoba 11, 2026 wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili, akiwa na umri wa miaka 92.

Wasifu wa Prof, Mmari

Prof. Mmari alizaliwa Moshi mkoani Kilimanjaro Juni 24, 1934 na kupata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Ilembula Mkoani Njombe mwaka 1940 mpaka 1946 na kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Ilboru, Arusha mwaka 1949 mpaka mwaka 1950.

Mwaka 1951 mpaka 1952 Prof. Mmari alijiunga na shule ya Sekondari ya Tabora (kwa sasa Tabora Boys). Mwaka 1953 -1956 alisoma Chuo Kikuu cha Makerere Uganda aliposomea Stashahada ya Ualimu.

Mwaka 1962, alijiunga na Chuo Kikuu cha Northern Iowa Cedar Falls Marekani, alisoma Shahada ya awali katika elimu na baadaye Shahada ya Uzamili (Masters), katika Elimu na kuhitimu mwaka 1964.

Alirejea nyumbani Tanzania mwaka 1968 na kujiunga na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumaliza mwaka 1974.

Baada ya kumaliza Shahada yake ya Uzamivu, Prof. Mmari aliendelea kushiriki katika mafunzo ya kozi fupi fupi ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Nigeria, Uingereza na Marekani kwa nyakati tofauti.

Mwaka 1957 katika shule ya  Sekondari Kahororo Bukoba, Mwaka 1958-1962 alifuundisha Ilboru Arusha na 1965 Tabora Sekondari. Mwaka 1970-1973 alikuwa Mdahiri Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1973-1974 alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu. Mwaka 1974-1977, Mkuu wa Idara ya Elimu, mwaka 1977-1982, Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii. Mwaka 1982-1984 Ofisa Mkuu wa Masuala ya Kitaaluma.

Aidha aliongoza taasisi nne za elimu ya juu na kuwa Makamu Mkuu wa vyuo vitatu Umma ambapo mwaka 1984 -1988 Chuo Kikuu cha Sokoine, 1988-1991 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mwaka 1993-2005. Mkuu wa Chuo cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARco) mwaka 2005 hadi alipostaafu mwaka 2013.

spot_img

Latest articles

TANESCO KUONGEZA UWEZO WA UPATIKANAJI WA UMEME KATAVI DISEMBA 1,2026-MD TWANGE

📌Aeleza Mpanda itakuwa na jumla ya megawati 80 na kukidhi mahitaji ya juu ya...

SERIKALI YAWASILISHA BUNGENI MKAKATI WA KUBORESHA UCHIMBAJI NA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Madini imewasilisha Bungeni mkakati kabambe unaolenga kufanya mabadiliko makubwa...

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA 10 WA MOESNA, KUWALETA PAMOJA MAWAZIRI 26

Na Tatu Mohamed TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 10 wa Kawaida wa Baraza...

MILIKI UBUNIFU MAJESHINI KULINDWA KISHERIA

Na Mwandishi Wetu AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni...

More like this

TANESCO KUONGEZA UWEZO WA UPATIKANAJI WA UMEME KATAVI DISEMBA 1,2026-MD TWANGE

📌Aeleza Mpanda itakuwa na jumla ya megawati 80 na kukidhi mahitaji ya juu ya...

SERIKALI YAWASILISHA BUNGENI MKAKATI WA KUBORESHA UCHIMBAJI NA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Madini imewasilisha Bungeni mkakati kabambe unaolenga kufanya mabadiliko makubwa...

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA 10 WA MOESNA, KUWALETA PAMOJA MAWAZIRI 26

Na Tatu Mohamed TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 10 wa Kawaida wa Baraza...