Tano za Yanga zamng’oa kocha Simba

Na Winfrida Mtoi, Media Brains

UONGOZI wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuachana na kocha mkuu wa kikosi hicho, Robertinho Oliveira kwa kuvunja mkataba wake wa miaka miwili aliotumikia kwa kipindi cha miezi 10.

Kocha huyo anaondoshwa ikiwa ni siku mbili tu baada ya kufungwa na watani zao Yanga mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Jumapili Novemba 5, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Robertinho raia wa Brazil, alijiunga na Simba Januari 3, 2023 akitokea Vipers SC ya Uganda na ameiongoza Simba katika michezo zaidi ya 25, ya Ligi Kuu Tanzania Bata na Kimataifa.

Katika Ligi Kuu tangu ametua nchini, amecheza mechi 18, akipoteza moja pekee dhidi ya Yanga huku akitoka sare mbili, huku akiipa Simba taji la Ngao ya Jamii alilotwaa msimu huu baada ya Wanamsimbazi hao kulikosa kwa misimu miwili mfululizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba, pia imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

“Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Selemani Matola. Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi  punde,” imesema taarifa hiyo.

spot_img

Latest articles

TMA yatoa mwelekeo wa mvua za Masika Machi hadi Mei 2026

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za...

Simba yataka Polisi iwashughulikie waliomkashfu bosi

Na Mwandishi Wetu KLABU ya Simba imeliandikia barua Jeshi la Polisi  ili kuwachukulia...

Waraka kwa Waziri Paul Christian Makonda

Katika dunia tunayoishi sasa michezo ni sekta inayoshikilia uchumi mkubwa. Wanamichezo wengi wamekuwa mabilionea...

ETDCO yaahidi kukamilisha Mradi wa Umeme katika vitongoji 372 Ruvuma kwa wakati

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji...

More like this