Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi

Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya kwenda kucheza michezo yao raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeelekea Angola, kuikabili  Wiliete ya nchini humo Septemba 19, 2025, Uwanja wa  11 de Novembro, huku Simba ikitarajiwa kutua Botswana ambapo  itacheza na Gaborone United Septemba 20, 2025 kwenye dimba la Obed Itani Chilume.

Vigogo hao wa soka nchini wenye maskani yao Kariakoo jijini Dar es Salaam, wameondoka baada ya jana kucheza mechi ya Ngao ya Jamii na Yanga kutwaa ubingwa huo.

Baada ya mechi hizo zitarejea nchini kujiandaa na michezo ya marudiano ambapo Yanga na Wiliete zitarudiana Septemba 27, 2025, Benjamin Mkapa.  Simba itarudiana na Gaborone United Septemba 28,2025 kwenye uwanja huo huo.

spot_img

Latest articles

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

More like this