Na Mwandishi Wetu
Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa ubingwa wa michuano ya Cecafa Kagame Cup kwa kuifunga Al Hilal mabao 2-1katika mchezo wa fainali uliopigwa leo Septemba 15, 2025, Uwanja wa KMC Complex Mwenye, Dar es Salaam.
Chama ametua Singida hivi karibuni baada ya kuachana na Yanga. Ubingwa huo ni wa kwanza katika historia ya timu hiyo, inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi.
Katika mchezo wa mapema APR FC ya Rwanda imeibuka mshindi wa tatu wa mashindano hayo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC FC.