CCM yaomba kuchangiwa bilioni 100 za kampeni

Na Mwandishi Wetu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinahitaji kupata sh 100 bilioni kwa ajili ya shughuli za kampeni kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waandishi na wahariri wa habari leo Agosti 11,2025, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCM ambaye pia ni mgombea mwenza wa Urais, Dk. Emmanuel Nchimbi ameviomba vyama shindani vya siasa kuichangia CCM sambamba na wanachama na wadau wengine.

Amesema harambee ya kuchangia kampeni za chama hicho inatarajia kuzinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya kampeni katika kugharamia magari, mabango, mafuta, fulana na kanga.

Dk. Nchimbi amesema uamuzi wa kuandaa harambee hiyo umetokana na hamasa kubwa iliyojitokeza kwa wanachama kutaka kuchangia kampeni.

“Kwa wakati ule kulitokea hamasa kubwa kwa wanachama wa CCM kutamani kuchangia michango ya kampeni. Kutokana na hamasa hiyo, sisi kama Kamati Kuu tumeamua sasa kuwashirikisha wanachama wetu katika uchangiaji kesho saa 11 jioni katika ukumbi wa Mlimani City,”


Vilevile, Dk. Nchimbi amefungua milango kwa vyama vingine kuchangia katika kampeni hiyo ambapo amesema kuwa;

“Kuhusu vyama vingine, tutafarijika sana vikichangia, kwa sababu haihitaji ushahidi wa kipolisi kujua CCM inatumikia watanzania na vyama vingine vyote,”

Akizungumzia kuhusu udhibiti wa fedha haramu, amesema “Jitihada yetu kubwa sisi kama CCM ni kujiepusha kuwa Serikali, kwa hiyo sisi siyo taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu. Wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha hizo, sisi tutaendelea kufanya kazi ya siasa, kwa maana kitu kinachoharibu nchi ni chama cha siasa kuendelea kufanya kazi za dola,” ameeleza.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...