Aliyerejeshwa awabwaga wapinzani wake Kunduchi, aongoza kura za maoni

Na Mwandishi Wetu

Mgombea wa udiwani Kata ya Kunduchi, jijini Dar es Salaam anayetetea nafasi yake Michael Urio ameibuka kinara katika kura za maoni kwa kuwabwaga wagombea wengine wa wanne kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Urio ambaye ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, awali jina lake halikurudi wakati wa uteuzi lakini baadaye alirejeshwa.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni yaliyotangazwa na msimamizi wa Kata hiyo leo Agosti 4, 2025 Urio ameongoza kwa kupata kura 257, anayefuatia Joyce Haule kura 250, Emmanuel Mkuchu hura 240, Hashemi Komba kura 30 na Happyness Justin alipata kura 12.

Urio ni miongoni mwa wagombea waliorejeshwa baada ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoa maelekezo kwa makatibu wa mikoa wa chama hicho kuwarejesha wagombea wote waliopitishwa na Kamati Siasa za mikoa ili wakapigiwe kura za maoni.

Kutokana na ushindi huo amejiweka katika nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea wa udiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this