Na Mwandishi Wetu
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kutumia nembo maalumu (QR Code) ya utambuzi wa taarifa zake ili kuzuia na kudhibiti uzushi na upotoshaji.
Kupitia taarifa iliyotolewa na chama hicho leo Julai 21, 2025, imesema kufahamu taarifa halisi ya vyanzo rasmi vya chama hicho utafanya uhakiki kwa ku- scan nembo hiyo.

“Taarifa yoyote ya uongo, ambayo watu wenye malengo ovu wanakuwa wameitengeneza kwa ajili kuzua tafrani na kupotosha jamii, msomaji aki- scan haiwezi kupelekwa, wala hawezi kuikuta kwenye vyanzo rasmi vya chama, iwe tovuti au kurasa za mitandao ya kijamii ya CCM,” imesema taarifa hiyo.