Na Mwandishi Wetu
TANGU kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari 1977 kwa muungano wa TANU na ASP, ChamaCha Mapinduzi (CCM) kimejidhihirisha kuwa ni chama kinachoongoza kwa uwezo wakutoa dira ya maendeleo, kulinda amani na mshikamano wa kitaifa na kutambuakikamilifu nafasi ya vijana katika ujenzi wa Taifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Chamakinaelekeza kuwa moja ya malengo yake makuu ni “kukuza na kudumishamshikamano wa kitaifa kwa njia ya demokrasia na usawa, bila kujali umri,jinsia wala kabila.”Katika misingi hii, CCM kimekuwa kikiwapa vijana nafasi ya kushiriki, kuongoza nakunufaika moja kwa moja na utekelezaji wa sera na Ilani ya uchaguzi.

Vijana hawajabakikuwa watazamaji, bali wamekuwa nguzo muhimu ya siasa, maendeleo na mageuzi yakijamii kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.
1. CCM NA HISTORIA YA KUWAJENGA VIJANA KUWA VIONGOZI WA TAIFA
Katika historia ya harakati za kisiasa nchini, vijana wamekuwa mstari wa mbele MwalimuJulius Nyerere alishiriki kuanzishwa TANU akiwa na umri wa miaka 32 na Mzee RashidKawawa akiwa na miaka 28 ,na uhuru wa Tanganyika umepatikana mwaka 1961 Mwalimu Nyerere akiwa na miaka 37.
Hii ni ishara tosha kuwa msingi wa mapambano ya uhuru namaendeleo ya taifa ulijengwa na vijana. CCM imerithi urithi huu kwa dhati na kuendelezamtazamo huo kwa vitendo tunaona kwa macho yetu kuwa CCM ni chama kinachowapafursa kubwa vijana na kinatambua mchango wa vijana.

Kwa mfano, kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), chama kimekuwa na chombomaalumu kwa ajili ya kuwaandaa vijana kitaaluma, kiitikadi na kiuongozi. Katiba ya CCMimetambua Jumuiya ya UVCCM kama mojawapo ya mihimili mitatu ya chama katikakukuza uongozi na ushiriki wa makundi maalum.
Miongozo ya chama inasisitiza kuwanafasi ya vijana si ya huruma bali ni haki na wajibu. Vijana wanashiriki katika vikao vyote vya maamuzi kuanzia ngazi ya tawi, shina, kata, wilaya, mkoa hadi taifa.
Mfano Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi katika ngazi yeyote ni mjumbe wa kikaocha kamati ya siasa, kikao cha halmashauri kuu kwa ngazi husika, hii inamaana vijanawanashiriki katika maamzui yote katika jamii.

2. ILANI YA CCM 2020-2025 NA 2025-2030 NI USHAHIDI WA KUJALI VIJANA KWA VITENDO
Katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020-2025 na ile ya 2025-2030, CCM imewekabayana mikakati thabiti ya kuwawezesha vijana. Baadhi ya hatua zilizotekelezwa naSerikali ya CCM chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni pamojana:-
➢ Ajira kwa Vijana: Zaidi ya ajira 8,084,203 zilitengenezwa kati ya 2020 hadi 2024, ambapo zaidi ya 7 milioni ni ajira zisizo rasmi.

Katika Ilani ya 2025-2030, CCM inalenga kuongeza kasi ya ajira kwa wastani wa asilimia 7 ya ukuaji wa uchumikwa mwaka.
➢ Mikopo kwa Vijana: Kupitia mapato ya Halmashauri, shilingi bilioni 96.3zilitolewa kwa vijana 8,242 kati ya 2020 hadi 2024. Hii ni pamoja na mikopo yenyemasharti nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
➢ Elimu na Mikopo ya Elimu ya Juu: Idadi ya wanafunzi wa elimu ya juuwalionufaika na mikopo iliongezeka kutoka 142,170 mwaka 2020 hadi 245,799mwaka 2024. Wanafunzi wa stashahada 9,959 walipata mikopo katika fani zenye kipaumbele.

➢ Samia Scholarship: Mpango huu umefadhili wanafunzi 3,696 katika masomo yasayansi, tiba, na uhandisi. Ni mpango unaodhihirisha jinsi Serikali ya CCMinavyowekeza katika rasilimali watu ya vijana.
➢ Elimu bila malipo kuanzia awali hadi kidato ha sita imekuwa ikitolewa ikiwapa fursa Watoto wa kitanzania na vijana kupata elimu bila kikwazo chochote.
CCM inaendelea kuwa na Imani kubwa sana vijana tumeshuhudia ziadiya salimia 50 vijana waeteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi kama wakuuwa wilya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa mikoa, mawaziri, wabunge.Chama cha mapinduzi kinatambua mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa.

3. HATUA ZA UCHUKUAJI FOMU NA FURSA ZA KISIASA KWA VIJANA
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM na kanuni zake, vijana wana nafasi zote sawa za kugombeanafasi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa , udiwani hadi ubunge, ili mradi tu wamekidhivigezo vya kikatiba.
CCM imefanya maboresho ya kanuni mnamo Machi 2025yaliyoongeza demokrasia na ushiriki wa vijana Wigo wa Kura za Maoni umeongezwa,Vijana wengi zaidi sasa wanashiriki kupiga na kupigiwa kura., Ukomo wa Viti Maalumkwa Wanawake umewekwa:
Hii imefungua nafasi zaidi kwa vijana wanawakekugombea majimbo au kata.Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, zaidi ya asilimia 60 yawaliochaguliwa katika maeneo mengi walikuwa vijana.
Huu ni ushahidi kuwa vijana waCCM wanaungwa mkono na wananchi na chama chao. Mfano mkoa wa Kigoma asilimia95 walioshinda uchaguzi wa serikali za mitaa walikuwa ni vijana
4. UTEKELEZAJI WA ILANI NA CCM KINAVYOGUSA MAISHA YA VIJANA NAWANANCHI KWA UJUMLA
Kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2025-2030:➢ Ajira na Uwezeshaji Kiuchumi: Serikali itaendelea kutoa mikopo yenyemasharti nafuu, kuimarisha huduma jumuishi za kifedha, na kuboresha mazingiraya biashara kwa vijana.
➢ Maendeleo ya Sayansi na TEHAMA: CCM inalenga kufundisha vijana ujuzi waTEHAMA, kuongeza matumizi ya teknolojia katika ajira, biashara na ubunifu.Michezo na Sanaa: Serikali ya CCM inakuza sekta ya sanaa na michezo kuwafursa ya ajira kwa vijana. Dkt. Samia alianzisha Tamasha la Sanaa la Samia (SamiaYouth Art Fund) na kuwekeza katika miundombinu ya michezo.
➢ Ruzuku ya Elimu na Elimu Bila Malipo: Shilingi trilioni 1.3 zilitumikakuendesha elimu bila ada kutoka awali hadi sekondari kati ya 2020-2024.
5. RAIS DKT. SAMIA NI MFANO HAI WA KIONGOZI ANAYEWAJALI VIJANA
Chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, CCM imeonyesha uthubutu na dira yakweli kwa kizazi kipya kizazi cha vijana. Dkt. Samia ameendelea kufungua milango yaajira, elimu, uwekezaji na diplomasia inayoleta fursa mpya kwa vijana.
Amekuwa Rais wakwanza mwanamke Tanzania, lakini pia kiongozi wa kwanza kuwateua vijana wengi kuwaWakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tawala na hata Mabalozi.
Kauli mbiu yake ya “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele” si maneno matupu, bali ni dira yenyeushahidi katika utekelezaji wa sera kwa vitendo.
HITIMISHO: CCM NI CHAMA CHA WOTE, LAKINI HASA CHA VIJANA
Kwa zaidi ya miaka 48 ya historia yake, CCM imejidhihirisha kuwa chama makini, kisasa,chenye mwelekeo wa kuandaa taifa la kesho kupitia uwekezaji katika vijana.
Kila kijana anayeamini katika maadili, uzalendo, na maendeleo ya kweli anapaswa kuona fahari nafursa ndani ya CCM.
Ni wakati wa vijana kuchukua fomu, kugombea kwa wingi, na kuhakikisha kuwa kura zaozinabeba matumaini yao. CCM sio chama cha historia tu, ni chama cha leo na kesho.