Makamu wa Rais atoa wito uboreshaji mfumo wa fedha

Na Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ametoa wito wa kufanyika maboresho ya mfumo wa fedha na ufadhili wa maendeleo duniani ili kutoa nafuu ya riba, kuwa endelevu, unaotabirika na unaozingatia usawa na vipaumbele vya mataifa yanayoendelea.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubia Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo (FfD4) unaofanyika Jijini Sevilla nchini Hispania.

Amesisitiza umuhimu wa mbinu za kibunifu katika ufadhili ikiwemo kubadili madeni ya kifedha kwenda katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile uhifadhi wa mazingira.

Vilevile Makamu wa Rais amesema taratibu za upimaji wa uwezo wa serikali kifedha katika ulipaji madeni unapaswa kupitiwa upya ili kuongeza uwazi na kuwa wa haki.

Ameongeza kuwa mkutano huo unapaswa kutoa ufumbuzi wa namna ya kupunguza gharama za ukopaji na kuongeza fursa za mikopo nafuu na ya muda mrefu.

Makamu wa Rais amesema kutokana na biashara kuwa nguzo ya kiuchumi ni vema mataifa kuwezeshwa katika uzalishaji na uongezawaji thamani wa bidhaa ili kufikia viwango vya kimataifa.

Amesisitiza uwepo wa usawa na haki katika taratibu na sheria za kibiashara za kimataifa ikiwemo masuala ya ushuru wa forodha na ukomo wa mauzo kwa mataifa yanayoendelea. Amesema unahitajika ushirikiano baina ya Mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea katika kuharakisha maendeleo ya sayansi, teknolojia na takwimu ili kuweza kusaidia katika utungaji sera na utekelezaji kwa kuzingatia tafiti na takwimu sahihi.

 Pia amesisitiza umuhimu wa Mataifa tajiri kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kupunguza viatarishi kwenye uwekezaji na ufadhili wa miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo.

Kuhusu Mazingira,ametoa wito wa kutoa kipaumbele katika ufadhili wa usimamizi na urejerezaji wa bioanuai pamoja na kuongeza wigo wa ufadhili katika miradi ya kujenga uhimilivu na miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesisitiza umuhimu wa kuanza kazi kwa mfuko wa mazingira wa kukabiliana na hasara na uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi (Loss and Demage Fund).

Makamu wa Rais amesema kufikia mwaka 2024, Tanzania imefikia asilimia 60 ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kupiga hatua zaidi katika lengo namba 2 hadi namba 7 hususani katika maeneo ya afya, utoshelevu wa chakula, elimu, usawa wa kijinsia, upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na upatikanaji wa nishati.

Ameeleza kuwa  ili kuendeleza mafanikio hayo unahitajika ushirikiano na ufadhili wa gharama nafuu katika kuongezea mapato ya ndani ya nchi.Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo unalenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika kugharamia utekelezaji wa SDGs, kujadili njia za kurekebisha mfumo wa fedha wa kimataifa ili kuwa jumuishi, wenye usawa na unaozingatia mahitaji ya nchi zinazoendelea.

Malengo mengine ya Mkutano huo ni pamoja na kupendekeza mbinu bora za kupunguza na kushughulikia mzigo wa madeni kwa nchi maskini na zenye kipato cha kati pamoja na kujenga mifumo madhubuti ya kifedha inayoweza kukabili athari za majanga ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Mkutano kuhusu Ufadhili wa Maendeleo ulianzishwa rasmi mwaka 2002 kupitia Mkutano wa kwanza uliofanyika Monterrey, Mexico na kupelekea kuundwa kwa msingi wa ushirikiano wa kimataifa katika kufadhili maendeleo.

spot_img

Latest articles

2020 Vunjo primaries leader to challenge Dr. Kimei again

Enock Koola (35), a staunch member of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party...

Esther Bulaya: Nilikuwa Chadema kwa mkopo nimerejea, CCM ni kama  Barcelona 

Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Kihongosi aahidi kutekeleza alichoagizwa na Rais Samia  Arusha

Na Mwandishi Wetu  Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha,  Kenani Kihongosi amesema  atafanya kazi aliyotumwa na Rais...

Rais Mwinyi aipongeza Yanga, aizawadia  milioni 100

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

More like this

2020 Vunjo primaries leader to challenge Dr. Kimei again

Enock Koola (35), a staunch member of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party...

Esther Bulaya: Nilikuwa Chadema kwa mkopo nimerejea, CCM ni kama  Barcelona 

Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Kihongosi aahidi kutekeleza alichoagizwa na Rais Samia  Arusha

Na Mwandishi Wetu  Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha,  Kenani Kihongosi amesema  atafanya kazi aliyotumwa na Rais...