Kaboyoka ajiunga rasmi na ACT Wazalendo

Na Tatu Mohamed

MBUNGE wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha 2020 hadi 2025, Nagy Livingstone Kaboyoka, amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo.

Hafla ya mapokezi imefanyika leo katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kaboyoka amepokelewa na Kiongozi wa Chama hicho, Ndugu Dorothy Semu, pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo.

Kaboyoka ni mzoefu katika siasa za Tanzania na amewahi kushika nafasi mbalimbali zenye ushawishi.

Alikuwa Mbunge wa kuchaguliwa wa Jimbo la Same Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kati ya mwaka 2015 hadi 2020, ambapo alimshinda aliyekuwa Mbunge wa CCM, Anne Kilango Malecela.

Aidha, amehudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa miaka 10 mfululizo, kuanzia mwaka 2015 hadi 2025.

Ujio wa Kaboyoka ndani ya ACT Wazalendo unaelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha nguvu ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, hasa katika harakati za kujenga upinzani imara na chenye dira ya uwajibikaji wa kweli kwa wananchi.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this