Uwekezaji magari ya umeme kuinufaisha Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Tanzania inatarajia kunufaika na matumizi ya magari yanayotumia umeme na gesi yanayotarajiwa kutengenezwa nchini kupitia kiwanda cha kampuni GF kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Hayo yameelezwa na Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey, wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Mahindra Scopion iliyofanyika Juni 21, 2025 jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Mahindra ni moja ya kampuni maarufu ya magari India na tayari imeingia Afrika hasa Tanzania, hivyo ujio wake utaleta mabadiliko makubwa kutokana na ubunifu wa teknolojia mpya katika utengenezaji wa magari.

Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Mahindra Scopion iliyofanyika Juni 21, 2025 jijini Dar es Salaam.

Amesema kutengenezwa kwa magari hayo Tanzania ni kutokana na kuimarika kwa mahusiani mazuri ya kibiashara kati ya India na Tanzania hali iliyowafanya wawekezaji wengi wa India kuwekeza nchini na moja wapo ni kampuni ya Mahindra.

“Mahindra ni moja ya kampuni maarufu ya utengenezaji ya magari aina ya Scorpion nchini India na sasa imeingia Tanzania, Uwekezaji wake utaleta manufaa makubwa kwa Tanzania na India kibiashara.

“Tuna furaha kuona ubunifu na teknolojia mpya ya utengenezaji magari inatumika Tanzania, kutengenezwa kwa magari haya mapya Tanzania yanakwenda kuondoa matumizi ya magari yaliyotumika kwa sababu ni bei nafuu na imara, naamini muda si mrefu tutashuhidia mabadiliko,” ameleeza Balozi Dey.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GF, Mehboob Karmali( katikati), akipongezana na Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey (kushoto),akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Mahindra Scopion iliyofanyika Juni 21, 2025 jijini Dar es Salaam.

Nae Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GF, Mehboob Karmali amesema ujio wa Mahndra nchini ni ukombozi kwani leo wametambulisha gari mpya sokoni na baadaye wataanza kutengeneza gari za umeme na gesi katika kiwanda chao likichopo Kibaha mkoani Pwani.

“Pia kwa kuanza tutaanza na magari madogo pickup- double cabin maalumu kwa shunguli za kilimo na wajasiliamali wadogo hasa mashambani. Ni gari ngumu ambazo zinakidhi shuhuli za kilimo vizuri. Mfano Zimbabwe watu wote wanatumia gari za Mahindra kwa ajili shambani.

Karmali amezitaka taasisi za umma na serikiali kwa jumla kujenga tabia ya kununu bidhaa kutoka viwanda vya ndani ili kuvilinda na kuongeza pato la Taifa na kuokoa pesa ambayo ingetumika kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Kampuni ya GF Automobile imezindua gari aina ya Mahindra Scorpion ambazo zina uwezo wa kustahimili mazingira ya barabara za aina yoyote hasa vijijini na mashambani, huku matumizi ya gesi yakiwa ni kulinda mazingira.

Magari hayo yanayotumia umeme na gesi yamekuja kipindi ambacho Serikali inahamasisha kuondokana na matumizi ya nishati chafu na kuingia katika matumizi ya nishati safi ili kulinda mazingira nakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...