Makanisa sita ya Gwajima yafungiwa  Mbeya

Na Mwandishi wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeyafungia matawi sita ya Kanisa la Ufufuo na Uzima yaliyokuwa yakiendelea  na huduma katika maeneo tofauti mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6,2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga  amesema kufungiwa kwa matawi hayo ni kunatokana na tamko la Serikali lililotolewa Juni 2, 2025 kupitia Msajili wa Jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa matawi ya Kanisa la Ufufuo na Uzima yaliyofungiwa ni pamoja na la lililopo ZZK katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi Mbeya vijijini pamoja na lililopo mtaa wa Mnadani katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali.

Mengine yaliyofungiwa ni yaliyopo katika Halmashauri za Wilaya za Chunya, Rungwe, Kyela pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Ameeleza kuwa bado ufuatiliaji unafanyika kuhakikisha wanayafungia wote na kuwataka viongozi na waumini  kuacha kuendesha  shughuli za vidimi katika makanisa hayo.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this