Na Mwandishi Wetu, Media Barains
Mamla ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza kuwa haihusiki na kufungwa kwa baa ya The Cask ya jijini Mwanza.
Taarifa iliyotolewa leo Agosti 17, na Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano imewataka wahusika kuwasiliana na mamlaka husika kuhusu jambo hilo.
“Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuujulisha umma kuwa, haijahusika kwa namna yoyote na ufungaji wa Bar ya THE CASK iliyopo jijini Mwanza.
“Tunaomba wahusika na umma wawasiliane na Mamlaka husika juu ya jambo hilo,” imeeleza taarifa hiyo ya TRA.
Agosti 16, mwaka huu taarifa kutoka jijini Mwanza zilidai kuwa Serikali wilayani Ilemela iliifunga baa hiyo kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili.
“Serikali wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeifunga baa maarufu ya The Cask Bar & Grill ya jijini Mwanza kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili.
“Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Kiomono Kibamba amesema, uongozi wa baa hiyo umekwapa kodi ya Serikali na kuendesha biashara zaidi ya moja eneo hilo hilo,” ilieleza taarifa hiyo.