Miaka 35 ya TAWLA yatamani mabadiliko zaidi ya Kisheria kwa Wanawake na Watoto

Na Tatu Mohamed

CHAMA cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kimeadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya kongamano maalum la kutafakari mafanikio, changamoto na mwelekeo wa baadaye wa chama hicho chenye mchango mkubwa katika kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto nchini.

Akizungumza leo Mei 22, 2025 katika kongamano hilo la siku mbili, Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipike amesema lengo kuu la mkutano huo ni kufanya tathmini ya safari ya chama hicho tangu kiliposajiliwa mwaka 1990 hadi sasa mwaka 2025, pamoja na kuweka mikakati ya mbele.

“Katika kujitafakari, tumeona ni muhimu kuchagua maeneo maalum ya haki ambayo kama chama tumeshayafanyia kazi au tunaweza kuyafanyia kazi kwa ufanisi zaidi. Maeneo hayo ni pamoja na haki za ardhi, magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na haki za watoto hasa tukitazama suala la mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia,” amesema.

Ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizokuwepo miaka ya nyuma kama mfumo dume, ambapo wanawake walikosa fursa za umiliki wa ardhi au kushiriki uongozi, mafanikio makubwa yamepatikana.

“Leo hii, Tanzania ina viongozi wa juu wanawake akiwemo Rais na Spika wa Bunge, jambo ambalo linaakisi mabadiliko chanya katika jamii.”Katika miaka hiyo ya mwanzo, tulikuwa na mawakili wanawake wasiozidi 10, leo hii ni zaidi ya 4000. Tumeona pia wanawake wakipenya katika taaluma nyingine kama uhandisi, na hata katika ngazi za Kata wanawake wengi sasa wanamiliki mali, wanafanya biashara na kushika nyadhifa za uongozi,” ameongeza.

Hata hivyo, TAWLA inasisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya, hasa katika mabadiliko ya sheria kandamizi.

Mkurugenzi huyo amesema wanatamani kuona Sheria ya Ndoa ikifanyiwa marekebisho ili ndoa iwe halali kuanzia umri wa miaka 18, na pia Sheria ya Elimu ijumuishwe kipengele kinacholinda haki ya mtoto wa kike aliyejifungua kurejea shuleni.

“Tungependa pia kuona sheria moja mahsusi kuhusu ukatili wa kijinsia, ambayo itarahisisha ufuatiliaji na utekelezaji wa haki,” amesema.

Hata hivyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi wanaowahitaji.

Kwa upande wake, Wakili Scholastica Ndyanabo amesema TAWLA inajivunia mafanikio yake ya miaka 35, hasa katika kuwasaidia wanawake na watoto kwenye masuala ya kisheria kama mirathi, migogoro ya ardhi na ndoa.

“Tumeweza kuwafikia watu zaidi ya milioni saba ndani na nje ya nchi. Wanawake na watoto ni makundi ambayo mara nyingi hayapewi kipaumbele cha huduma za kisheria, na sisi kama taasisi tumejikita kuwapa msaada huo muhimu,” amesema Ndyanabo.

Katika kuadhimisha miaka hii 35, TAWLA haijajikita tu katika kusherehekea mafanikio, bali imejielekeza katika kupanga hatua madhubuti za kusukuma mbele ajenda ya haki za wanawake na watoto kwa miongo ijayo.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...