Jeshi la Polisi lamkamata kiongozi wa Chadema

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemkamata Naibu Katibu Mkuu  Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Aman Golugwa kwa uchunguzi wa tuhuma za kusafiri kwa siri kwenda na kurudi nje ya Tanzania.

Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa  leo  Mei 13, 2025 imesema Golugwa amekamatwa saa 6:45 usiku Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels nchini Ubelgiji.

“Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa nchini,”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhusu suala hilo.”

Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomuhusu Golugwa.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this