Simba yaizindua Serikali ukarabati uwanja wa Mkapa, mkandara apewa maagizo

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemuagiza mkandarasi anayesimamia ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuhakikisha maeneo muhimu ya uwanja huo yanakamilika ifikapo Mei 10, 2025 ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na RS Berkane.
 
Agizo hilo amelitoa leo Aprili 29, 2025 katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati huo hususan eneo la kuchezea  ambalo linahitajika kuwa bora kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Mei 25,2025.

Amesema  Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imetoa maelekezo maalum kuhakikisha Watanzania wanashuhudia historia ya kipekee, kwani mara ya mwisho fainali ya CAF ilichezwa Tanzania ilikuwa ni mwaka 2023 ambapo Yanga walicheza fainali, na kabla yake mwaka 1993 Simba walifika hatua hiyo.

“Tunataka Watanzania wajivunie, wajione sehemu ya historia. Kombe linakuja hapa nyumbani na tunataka uwanja huu uwe tayari kulipokea,” amesema.
 
Ameongeza  kuwa, uwanja unapaswa kuwa tayari kwa watazamaji zaidi ya 63,000 kushuhudia tukio hilo la kihistoria, ingawa changamoto kubwa iliyojitokeza ni ubora wa sehemu ya kuchezea hasa baada ya mechi ya robo fainali kati ya Simba na Al Masry, hivyo eneo hilo linapewa kipaumbele cha ukamilishaji.
 
Ametoa maelekezo ya ukarabati wa miundombinu mingine muhimu ndani ya uwanja huo, ikiwemo kukamilisha sehemu ya benchi la ufundi la waamuzi kwa kuweka mataili, kuweka viti vya muda katika sehemu zilizo wazi, na kuhakikisha ifikapo Ijumaa kazi hizo ziwe z

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this