Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yajizatiti kuboresha uwezo wa mawakili wa Serikali

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imejipanga katika kuendelea kuimarisha na kuboresha uwezo wa Mawakili wa Serikali nchini.

Hayo yamesemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari wakati akizungumza na kwenye Mkutano maalumu na vyombo vya habari uliofanyika Machi 19, 2025 katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kivukoni Jijini, Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mafunzo maalumu kwa Mawakili wa Serikali nchini yatakayofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 24 hadi 28, 2025 yakiwa na lengo la kuongeza umahiri na utendaji kazi wa Mawakili hao.

Mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali ni sehemu ya kuimarisha utaratibu wa Mafunzo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mawakili hao, pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika mapema mwezi Febuari, 2025 ambapo aliiagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuboresha na kuimarisha utendaji kazi wa Mawakili wa Serikali.

“Rais amekuwa akisisitiza mara kwa mara kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha inaboresha na kuimarisha uwezo wa Mawakili wa Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha, Johari ameeleza kuwa Mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali yataendeshwa na wakufunzi wabobezi wa ndani na nje ya nchi, ambao watatoa mada mbalimbali zitakazo waimarisha mawakili hao katika Uandishi, Uingiwaji na Majadiliano ya Mikataba ya Kimataifa, Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara, na Uandishi wa Sheria.

“Kama mnavvofahamu Rais anazidi kuifungua nchi, wigo wa uwekezaji unaizidi kupanuka hivyo sisi kama Wanasheria ni lazima tuhakikishe kwamba tunanyumbulika ili kuendana na kasi hiyo,” ameeleza Johari.

Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Mafunzo hayo yatatoa fursa kwa Mawakili wa Serikali kujifunza zaidi majukumu yao katika kuuvaa uzalendo na kulinda maslahi na usalama wa Taifa, ili waweze kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya Taifa na kuzingatia Usalama wa nchi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa, Mafunzo hayo yatawasaidia Mawakili wa Serikali kuweza kujikumbusha Sheria zinazohusu foreign exchange, hati fungani na dhamana.

“Tunataka kuwa na Wanasheria na Mawakili ambao watakuwa na uelewa mzuri katika masoko ya fedha, masoko ya mitaji,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Vilevile Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa wito kwa Mawakili wa Serikali nchi nzima kuhudhuria bila kukosa mafunzo hayo, huku akiziomba Wizara, Taasisi na Halmashauri kuwaruhusu na kuwawezesha Mawakili wa Serikali kushiriki katika mafunzo hayo kwani yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.

“Nitoe wito kwa Mawakili wa Serikali ambao hawajajisajili wafanye hivyo haraka sana ili waweze kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatawasaida kuimarisha utendaji kazi wao,” amesema Johari.

Sambamba na hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitumia Mkutano huo na Vyombo vya Habari kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya Uongozi wake pamoja na mafanikio makubwa ambayo Taifa imeweza kuyapata.

spot_img

Latest articles

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

Shirika la Posta Tanzania lashiriki kongamano la eLearning Afrika, laja na huduma ya Swifpack

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Posta Tanzania ni miongoni mwa washiriki katika kongamano la...

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

More like this

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

Shirika la Posta Tanzania lashiriki kongamano la eLearning Afrika, laja na huduma ya Swifpack

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Posta Tanzania ni miongoni mwa washiriki katika kongamano la...