Derby ya wanawake kesho, ubabe ubabe

Na Winfrida Mtoi

Simba Queens na Yanga Princess kesho Machi 18,2025 zinashuka dimbani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Kila mmoja akionekana kuwa na hamu ya  kuondoka na alama zote tatu ambapo Yanga Princess inahitaji kulipa kisasi ya kipigo cha bao 1-0 ilichopokea katika mechi ya mzunguko wa kwanza, huku Simba Queens ikitaka kuendeleza ubabe mbele ya wadada hao wa Jangwani.

Simba Queens ambayo ni mwenyeji wa mchezo huo, inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 34 wakati Yanga ikiwa nafasi ya tatu na alama 24 zote zikicheza mechi 12.

Akizungumzia mchezo huo kocha mkuu wa Simba Queens, Yussif Basigi amesema ni mechi muhimu kwao kutokana na kila mmoja kuitolea macho, huku akihitaji ushindi ili kuendelea kukaa kileleni kwa sababu wamepishana alama mbili na JKT Queens iliyopo nafasi ya pili.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema, ametamba kuwa licha ya wapinzani wao kuwa kwenye ubora na kuongoza ligi lakini  wamejiandaa vizuri na hawana presha.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this