Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) Catherine Russell, leo Machi 11, 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia ameishukuru UNICEF kwa mchango wake katika masuala mbalimbali ikiwemo afya, elimu na lishe kwa watoto pamoja na afya ya msingi.


