Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura Dar kuanza Machi 17

Na Mwandishi Wetu

UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam utafanyika kwa siku saba kuanzia Machi 17 hadi 23, 2025 ambapo wapiga kura wapya 643,420 wanatarajiwa kuandikishwa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Machi, 2025.

“Leo tupo hapa Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huu, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 17 Machi, 2025 na kukamilika tarehe 23 Machi, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema mkoa wa Dar es Salaam ndio wa mwisho kwenye awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Dafatri ambayo ilizinduliwa mwezi Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika kwenye mikoa 28 na kwamba mikoa ya Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga inatarajiwa kukamilisha zoezi hilo tarehe 07 Machi, 2025.

“Hadi leo tarehe 05 Machi, 2025 Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 28. Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Aidha, zoezi la uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa wa Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga unaendelea tangu tarehe 01 Machi, 2025 na utakamilika tarehe 07 Machi, 2025,” amesema Jaji Mwambegele.

Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

spot_img

Latest articles

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

More like this

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...