Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa Mkurugenzi mpya wa Kanda ya Afrika atachaguliwa Mei mwaka huu.
Uteuzi huo unakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi mteule wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile aliyefariki dunia Novemba 27, 2024 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kutokana na kifo chake, WHO imeamua Mataifa yateue tena wagombea, huku tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ikiwa Februari 28, mwaka huu.
Dkt. Tedros Ghebreyesus ametangaza kuwa mchakato wa kura utafanyika Mei 8, 2025 na jina la kiongozi mpya litapitishwa rasmi Agosti 2025.
Aidha WHO imemteua Dkt. Chikwe Ihekweazu kama Kaimu Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika.