Wizara ya Afya Somalia yaichagua Tanzania kushirikiana kwenye ugavi wa bidhaa za afya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Afya nchini Somalia imeichagua Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora.

Hayo yamebainishwa na watendaji wa Wizara ya Afya kutoka nchini Somalia waliotembelea Bohari ya Dawa (MSD), ambapo mwakilishi wa ugeni huo Mohamed Abdulukadiri Hersi ameeleza kuwa hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia MSD katika mifumo inayotumika katika mnyororo mzima wa ugavi inayotumia teknolojia ndio umewavutia zaidi kuja kujifunza.

“Tumeamua kuja Tanzania kujionea namna inavyofanya kazi pamoja na kuona mifumo mingine ya serikali. Somalia ipo kwenye mpango wa kujenga upya mfumo wake wa ugavi wa bidhaa za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kufikisha bidhaa za afya kwa wananchi.

“Hivyo kati ya Nchi tulizochagua kuwa mfano ni Tanzania, ambapo kupitia MSD tumejifunza mengi ambayo tutakwenda kuyatekeleza tutakaporudi,” amesema Hersi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, ameeleza kuwa wageni hao wamekuja Tanzania kwa muda muafaka ambapo MSD imefanya mageuzi makubwa ya kiutendaji ikiwemo kujiendesha kibiashara, na kufanya maboresho mbalimbali katika mnyororo mzima wa ugavi wa bidhaa za afya, hivyo watajifunza mengi.

spot_img

Latest articles

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

More like this