Lugalo yang’ara  shindano la gofu

Na Winfrida Mtoi

Klabu ya Lugalo imeng’ara katika shindano la gofu la  Vodacom Lugalo Open 2024 baada ya mchezaji wa klabu hiyo, Prosper Emmanuel kuibuka mshindi wa jumla wa shindano hilo kwa gross 225.

Mshindi wa pili ni Samweli Kileo akishinda kwa gross 226, watatu Isika Daud gross 229 wote wakitokea katika klabu hiyo, huku mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa akiwa ni Nuru Morel kutoka Arusha Gymkana kwa gross 147.

Shindano hilo la siku tatu lilihusisha  zaidi ya wachezaji 200 kutoka katika klabu mbalimbali kwa kushikisha vijana, wanawake na watu wazima.

Akizungumza wakati wa kufunga shindano hilo, Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ameipongeza klabu ya Lugalo kwa kuwa chachu ya kuendeleza mchezo huo kutokana na kuandaa mashindano mbalimbali na uwepo wa miundombinu bora inayoruhusu mchezo huo kuchezwa muda wowote.

Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akipiga mpira katika shindano la gofu kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo. 

“Nawapongeza sana  Lugalo Golf Klabu, imekuwa ni klabu ambayo inazingatia ubora na viwango, ukifika Lugalo unahisi wewe kweli ni mchezaji, kila kitu kinakuwa  kipo katika ubora unaotakiwa,” amesema.

Aidha Dk. Ndumbaro ameeleza kuwa mustakabari wa mchezo huo upo kwa vijana na wizara yake imepeleka wazo serikalini na limekubaliwa ambapo kuanzia mwakani mchezo wa gofu utachezwa kwenye mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA.

spot_img

Latest articles

Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na...

Rais Mwinyi azindua Baraza la Wawakilishi, ataja mwelekeo wa Serikali atakayounda

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

More like this

Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na...

Rais Mwinyi azindua Baraza la Wawakilishi, ataja mwelekeo wa Serikali atakayounda

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...