Katibu Mkuu Uwekezaji afanya ziara Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais – Uwekezaji, Dk. Fred Msemwa, leo Machi 4, 2026, ametembelea Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) kwa ziara ya kujitambulisha kufuatia kuteuliwa kwake na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika wadhifa huo.

Ziara hiyo ya Dk. Msemwa, aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Februari 6, 2026, ilianza kwa mapokezi rasmi OMH, jijini Dar es Salaam, ikifuatiwa na utambulisho wa menejimenti.

Dkt. Msemwa alitembelea maeneo mbalimbali ya kazi na kujionea mazingira ya utendaji pamoja na mifumo inayotumika katika kusimamia uwekezaji wa Serikali na rasilimali za umma.

Katika kikao cha pamoja na menejimenti, alipokea wasilisho la kina lililoelezea muundo wa taasisi, majukumu ya kisheria, utekelezaji wake, mafanikio yaliyopatikana na mipango ya muda mrefu ya kimkakati.

Wasilisho hilo lilibainisha mchango wa taasisi za umma katika kuongeza mapato ya Serikali, kuimarisha nidhamu ya matumizi na kuongeza tija katika uwekezaji wa umma.

Akizungumza baada ya wasilisho hilo, Dkt. Msemwa aliipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa utendaji mzuri na mageuzi yanayoendelea, hususan katika kuimarisha mchango wa taasisi za umma katika uchumi wa taifa.

Alisisitiza usimamizi madhubuti wa rasilimali za umma, uwazi, na uwajibikaji kama misingi ya kujenga uchumi imara na endelevu.

Aidha, aliahidi ushirikiano wa karibu katika kutatua changamoto zozote zinazoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, ambaye alikuwa mwenyeji wa ziara hiyo, alimshukuru Katibu Mkuu kwa kutenga muda wa kutembelea ofisi hiyo.

Alieleza kuwa ziara hiyo ni ishara ya kuimarisha mshikamano wa kiutendaji na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya taasisi.

Bw. Mchechu aliahidi kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili kuhakikisha kila taasisi inatekeleza wajibu wake kwa ufanisi, akisisitiza kuwa kujenga wizara imara kunaanzia katika kuzijenga taasisi zilizo chini yake kuwa imara, zenye uwajibikaji na zinazozingatia matokeo.

Alibainisha kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Ofisi ya Rais – Uwekezaji na Ofisi ya Msajili wa Hazina utaongeza ufanisi wa usimamizi wa uwekezaji wa Serikali na kulinda maslahi ya taifa.

Ziara hiyo imeimarisha mahusiano ya kikazi na kuweka msingi wa ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuongeza tija, uwazi na mchango wa taasisi za umma katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...