Chadema yaongoza maandamano Arusha

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaongoza Maandamano ya amani jijini Arusha, likiwa ni hitimisho la awamu ya kwanza ya maandamano yaliyoogozwa na chama hicho katika mikoa minne nchni.

Tayari chama hicho kimefanya maandamano kama hayo katika makao makuu ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya. Maandamano hayo yanaonozwa na viongozi wakuu wa chama hicho, wakiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe, Maksmu Mwenyekiti (Bara), Tundu Lissu na Katibu Mkuu, John Mnyika. Kwa mujibu wa Msimamizi wa maandamano ya Kanda ya Kaskazini, Salum Mwalimu maandamano hayo nayatarajiwa kuhitimishwa alasiri kwa mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika uwanja wa reli.

Lengo la maandamano hayo yaliyopewa jina la ‘vuguvugu la haki ya Watanzania’ ni kuishinikiza Serikali kushughulikia tatizo la gharama za maisha. Pia, kuitaka Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kwenye miswada ya uchaguzi iliyokuwa imepelekwa bungeni Novemba 10 mwaka jana na kujadiliwa katika mkutano wa bungeni kisha kupitishwa na sasa inasubiriwa kusainiwa na Rais kuwa sheria.

Maandamano hayo yalianzia jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN), zilizopo Ubungo, kufikisha ujumbe wao huo, wakati yale ya jijini Mwanza yalimalizika kwa mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha na jijini Mbeya yalihitimisha pia kwa mkutano kama huo Viwanja vya Rwanda Nzovwe.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this