Mlugu Mtanzania wa kwanza kutinga robo fainali mashindano ya Judo Jumuiya ya Madola 2026

Glasgow, Scotland

Mchezaji wa Judu, Andrew Mlugu, ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola 2026 yaliyofanyika Glasgow, Scotland kuanzia Julai 23 hadi Agosti 2, 2026.

Mlugu alihitimisha safari yake katika mashindano hayo baada ya kuishia hatua ya robo fainali katika uzani wa kilo 81.

Mchezaji huyo alianza vyema mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi wa Ippon dhidi ya Jamison Dick wa Ushelisheli katika hatua za awali, ushindi uliompa tiketi ya kutinga robo fainali.

Katika robo fainali, alikabiliana na Keishin Ochi wa Australia, ambapo alipoteza kwa Ippon. Hata hivyo, kutokana na mfumo wa mashindano, alipata nafasi ya kuendelea kupitia hatua ya Repechage, akiendelea kuwania medali ya shaba.

Katika pambano la Repechage, Mlugu alikutana na Fernand Nkero wa Gabon, lakini juhudi zake hazikutosha baada ya kupoteza kwa alama 2-0, matokeo yaliyohitimisha safari yake kwenye mashindano hayo.

Licha ya kutofika hatua za medali, Mlugu ameonesha kiwango kizuri cha ushindani, ujasiri na uzalendo kwa kupambana dhidi ya wapinzani wenye uzoefu mkubwa kutoka mataifa mbalimbali.

spot_img

Latest articles

FURSA ZA BIASHARA ZA MABILIONI KATIKA MIGODI ZAWAFUNGUKIA WATANZANIA

Vijana na wanawake wapewa kipaumbele kunufaika na mnyororo wa thamani wa madini Na Mwandishi Wetu...

GST yaongeza kasi ya tafiti za kijiosayansi kuvutia uwekezaji sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeongeza kasi ya...

UDSM wabuni mfumo wa simu janja unaosaidia wakulima kutumia maji kwa ufanisi

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimebuni mfumo wa kidijitali unaotumia...

UDSM yahamasisha uwekezaji katika ufugaji wa nyuki wasiodunga

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesema Tanzania ina fursa...

More like this