GST: Taarifa sahihi za kijiolojia ni msingi wa uchimbaji wenye tija

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imewataka wachimbaji, wawekezaji na wananchi kutumia huduma za kitaalamu za kijiolojia kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji wa madini, ikisema hatua hiyo itapunguza gharama za uwekezaji, kuongeza uwezekano wa kugundua madini na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.

Akizungumza katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima ‘Nanenane’ yanayoendelea jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa GST, Neema Mhagama, alisema taasisi hiyo imejizatiti kutoa taarifa sahihi za kijiolojia zinazowasaidia wachimbaji kufanya maamuzi yenye tija badala ya kutegemea kubahatisha wanapofungua migodi.

Amesema GST ina wataalamu wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu wanaofanya tafiti za kijiolojia na kutoa taarifa zinazowawezesha wawekezaji kufahamu maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kuwa na rasilimali za madini kabla ya kuwekeza fedha nyingi katika uchimbaji.

“Matumizi ya taarifa sahihi za kijiolojia yanaongeza ufanisi wa shughuli za uchimbaji, hupunguza hatari za uwekezaji na kuongeza tija kwa wachimbaji pamoja na mapato ya Serikali,” amesema Mhagama.

Ameeleza kuwa GST imeendelea kuimarisha uwezo wa wataalamu wake kupitia mafunzo ya ndani na nje ya nchi pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za kimataifa, zikiwemo taasisi za jiolojia za Finland na Korea, hatua ambayo imeongeza ubora wa tafiti na huduma zinazotolewa.

Mhagama amesema wananchi na wadau wa sekta ya madini wanaofika katika makao makuu ya GST wanaweza kupata huduma mbalimbali za kitaalamu, ikiwemo taarifa za kijiolojia, ushauri wa kitaalamu, pamoja na maktaba yenye tafiti na nyaraka muhimu zinazohusu rasilimali za madini nchini.

Amesisitiza kuwa uwekezaji unaozingatia taarifa za kisayansi huchangia matumizi bora ya rasilimali, hupunguza hasara zinazotokana na uchimbaji usio na taarifa sahihi na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa Mhagama, ushiriki wa GST katika Maonesho ya Nanenane unalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo pamoja na kuonesha nafasi ya taarifa za kijiolojia katika kuchochea maendeleo ya sekta ya madini na shughuli nyingine za uzalishaji, ikiwemo kilimo.

Amewataka wachimbaji wadogo, wawekezaji na wananchi wanaotaka kuingia katika sekta ya madini kutumia fursa ya maonesho hayo kutembelea banda la GST ili kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa, au kufika katika ofisi za taasisi hiyo kwa ushauri wa kitaalamu utakaowawezesha kufanya uwekezaji wenye tija, kuongeza uzalishaji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

spot_img

Latest articles

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...

TANESCO YAELEZA MIKAKATI YAKE YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA WAKATI WA MVUA ZA EL NINO

📌Yaelimisha wananchi kuchukua tahadhari katika matumizi salama ya umeme kipindi cha mvua Na Mwandishi Wetu...

More like this

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...