TANESCO YAELEZA MIKAKATI YAKE YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA WAKATI WA MVUA ZA EL NINO

📌Yaelimisha wananchi kuchukua tahadhari katika matumizi salama ya umeme kipindi cha mvua

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza mikakati mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kukabiliana na athari za mvua za El Nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya umeme pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya umeme wakati wa mvua.

TANESCO imeeleza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kupatikana kwa usalama na kwa uhakika, huku wananchi wakichukua tahadhari dhidi ya hatari inayoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.

Hayo yameelezwa katika mahojiano maalumu na wataalamu mbalimbali wa TANESCO yaliyofanyika katika vipindi mbalimbali vya Radio na Televisheni, kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu maandalizi na mikakati ya TANESCO katika kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

Akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Media, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, amesema Shirika linaendelea na hatua mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya umeme ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Nino.

“Kwa sasa TANESCO inaendelea na ukaguzi na uimarishaji wa miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo kubadilisha nguzo zilizoharibika na kuweka nguzo imara, kukagua hali ya nyaya za umeme, pamoja na kukata miti inayokaribia au kugusa njia za umeme,” amesema Bi. Gowelle.

Ameongeza kuwa TANESCO pia inaendelea kukagua vituo vya kupokea na kupoza umeme pamoja na mazingira yanayozunguka miundombinu hiyo, hatua inayolenga kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa umeme unaendelea kuwa salama katika kipindi cha mvua.

Kwa upande wake, Meneja wa Afya na Usalama Kazini , Mhandisi Fred Kayega, amesema maji na vitu vyenye asili ya chuma vinaweza kurahisisha upitishaji wa umeme, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini zaidi wakati wa mvua na mafuriko.

“Tunasisitiza wananchi kutogusa nyaya za umeme zilizoanguka chini, hasa wakati wa mvua au mafuriko. Wananchi wanapaswa kujiweka mbali na eneo hilo na kutoa taarifa TANESCO ili wataalamu wafike na kuchukua hatua za haraka ,” amesema Mhandisi Kayega.

TANESCO inaendelea kuwahimiza wananchi kushirikiana na Shirika kwa kutoa taarifa mapema wanapoona miundombinu ya umeme iliyo katika hali isiyo salama, ikiwemo nguzo, nyaya zinazoning’inia au kuanguka chini, pamoja na miti inayoonekana kugusa Nyaya au nguzo za umeme ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

spot_img

Latest articles

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...

IDARA YA UTAFITI, MIPANGO NA UWEKEZAJI TANESCO WAASWA KUFANYA KAZI KWA UBUNIFU

📌 Wapongezwa kwa mafanikio ya miradi 📌Watumishi watakiwa kuongeza kasi, teknolojia na matumizi ya wataalamu...

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

More like this

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...

IDARA YA UTAFITI, MIPANGO NA UWEKEZAJI TANESCO WAASWA KUFANYA KAZI KWA UBUNIFU

📌 Wapongezwa kwa mafanikio ya miradi 📌Watumishi watakiwa kuongeza kasi, teknolojia na matumizi ya wataalamu...