Wanaotuhumiwa kuiba vifaa Lumo sekondari mikononi mwa Takukuru

Na Nora Damian

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwachukulia hatua watu saba wanaodaiwa kuiba vifaa vya ujenzi katika Shule ya Sekondari Lumo iliyopo Wilaya ya Temeke.

Chalamila amewataja watu hao (majina tunayahifadhi) leo Februari 20,2024 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Lumo Wilaya ya Temeke.

Taarifa za ndani zinasema baadhi ya wanaotuhumiwa ni wenyeviti wa serikali ya mtaa na viongozi wa CCM wa tawi.

“Kwenye vitu vya msingi hatutaki mchezo na walioshiriki wengine ni watu wetu. Alichoiba sio CCM bali ni mali ya Watanzania.

“Miradi anayoijenga Rais Samia kila mmoja aione kama maji ya betri ambayo hawezi kupigia mswaki au kufanyia chochote….lazima vifaa hivyo virudi haraka iwezekanavyo,” amesema Chalamila.

Kabla ya mkutano huo Chalamila alifanya ziara katika shule hiyo na kukagua mradi huo wa ujenzi wa vyumba 32 vya madarasa ya ghorofa, ofisi za walimu 16, matundu ya vyoo 96 ambao unagharimu Sh bilioni 2.4.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Lumo, Frida Kyando, amesema mpaka sasa fedha zilizopokelewa ni Sh bilioni 1.6 na zilizotumika ni Sh bilioni 1.1.

Kwa mujibu wa mkuu huyo kati ya fedha hizo mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ni Sh bilioni 1 na Serikali Kuu Sh milioni 640.

Amesema mradi huo utakapokamilika utapunguza msongamano wa wanafunzi na kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kusoma ndani ya Kata ya Yombo Vituka ambapo ni karibu na makazi yao.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga, amesema hawako tayari kuona Rais Samia anadhalilishwa na watu wasio waaminifu na kusisitiza waliohusika wachukuliwe hatua wakiache chama kikiwa salama.

spot_img

Latest articles

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

Chondechonde Polisi msisababishe wananchi wakate tamaa

ALHAMISI iliyopita yaani Desemba 5, mwaka huu wa 2024 lilitokea tukio baya la kuhuzunisha...

Ufaransa yaipatia Tanzania Sh bilioni 323.4

Na Mwandishi Wetu Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba...

TANZANIA YAWEKA REKODI MKUTANO WA WAHASIBU WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi Wetu Tanzania imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali...

More like this