TANESCO YATIMIZA AHADI: YAFUNGA TRANSFOMA KUONDOA KERO YA UMEME KATAVI

📌Utekelezaji huo unafuatia maagizo ya Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyetoa muda hadi Desemba 01, 2026.

📌TANESCO yakamilisha kazi Jumapili ya Novemba 15, 2026 ikiwa ni kabla ya muda ilioagizwa.

📍 Mpanda, Katavi | Novemba 24, 2026

Na Mwandishi wetu,

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetekeleza maagizo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa kufunga transfoma mpya na kubwa yenye uwezo wa MVA 150 katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Ibadakuli mkoani Shinyanga, hatua inayolenga kumaliza kabisa changamoto ya upungufu wa umeme mkoani Katavi.

Hatua hiyo ni matokeo ya ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais aliyoifanya Oktoba 13, 2026 mkoani Katavi, ambapo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, kuhakikisha TANESCO inaboresha hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Katavi ifikapo tarehe 01 Desemba, 2026 ambapo TANESCO imekamilisha Jumapili ya Novemba 15, 2026.

Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Katavi baada ya marekebisho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mhe. Idd Kimanta amesema Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Bw. Lazaro Twange aliahidi mbele ya Makamu wa Rais hadi kufikia Disemba moja Mkoa wa Katavi utakuwa na umeme wa uhakika.

“Shukrani za wanakatavi zimwendee Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kwa kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais kwa haraka sana chini ya muda ambao alituahidi wana Katavi”. Amesema Mhe. Kimanta.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi, Mha. Florence Mwakasege amesema upatikanaji wa umeme Mkoa wa Katavi kwa hivi sasa umeimarika na kutoa rai kwa wananchi kuendelea kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kwani upo wa kutosha.

“Ilikuwa ikifika saa kumi na moja jioni au saa mbili usiku umeme unakatika kwa muda mfupi kutokana na kuzidiwa na mahitaji, lakini kwa hivi sasa changamoto hiyo imeisha baada ya kufunga transfoma kubwa ya MVA 150 kituo cha umeme cha Ibadakuli mkoani Shinyanga”. Amesema Mha. Florence.

Akiongea kwa niaba ya Wafanyabiashara Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Katavi, Bw. Aman Mahela ameipongeza TANESCO kwa kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais kabla ya wakati ambao walikuwa wamepangiwa na kuhakikisha Mkoa wa Katavi unakuwa na umeme wa uhakika.

“Wafanyabiashara wa Katavi tunashukuru na kuwapongeza TANESCO kwa kukamilisha kazi hiyo kabla ya muda ambao umepangwa, natoa rai kwa wafanyabiashara wenzangu kuendelea kuiamini Serikali na inafanya kazi ya kuhudumia wananchi kwa wakati”. Amesisitiza Bw. Mahela.

TANESCO ilianza kazi ya kufunga transfoma hiyo ya MVA 150 tangu Oktoba 27, 2026 na kukamilika Jumapili ya Novemba 15, 2026.

Kituo cha Ibadakuli ndicho kinacholisha umeme katika mikoa ya Tabora na Katavi. Kukamilika kwa ufungaji wa transfoma hiyo kunaongeza kiwango cha umeme kinachofika katika Manispaa ya Mpanda na maeneo jirani.

spot_img

Latest articles

UZALISHAJI GESI ASILIA WAFIKIA FUTI ZA UJAZO BILIONI 65.4, PURA YAOKOA SH BILIONI 8.86

Na Tatu Mohamed UZALISHAJI wa gesi asilia nchini umeongezeka na kufikia futi za ujazo bilioni...

MIRADI YA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME DAR ES SALAAM YAFIKIA HATUA ZA MWISHO KUKAMILIKA – MD TWANGE

📌Serikali yawekeza zaidi ya bilioni 193 kuimarisha upatikanaji wa umeme Dar kukidhi ongezeko la...

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA TUME ZA UCHAGUZI ECF-SADC

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan...

NESCH MINTEC YAPUNGUZA GHARAMA ZA VIPIMO VYA MADINI KUPITIA MAABARA YA MWANZA

Na Mwandishi Wetu WACHIMBAJI na wafanyabiashara wa madini nchini sasa wana fursa ya kupata...

More like this

UZALISHAJI GESI ASILIA WAFIKIA FUTI ZA UJAZO BILIONI 65.4, PURA YAOKOA SH BILIONI 8.86

Na Tatu Mohamed UZALISHAJI wa gesi asilia nchini umeongezeka na kufikia futi za ujazo bilioni...

MIRADI YA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME DAR ES SALAAM YAFIKIA HATUA ZA MWISHO KUKAMILIKA – MD TWANGE

📌Serikali yawekeza zaidi ya bilioni 193 kuimarisha upatikanaji wa umeme Dar kukidhi ongezeko la...

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA TUME ZA UCHAGUZI ECF-SADC

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan...