Na Mwandishi wetu- Dodoma
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kutumia mifumo ya kisasa kusimamia uendelezaji wa Mji wa serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 24 Novemba, 2026 jijini Dodoma katika Kikao cha Kumpitisha kuhusu kuimarisha usimamizi ujenzi uendeshaji wa Mji wa Serikali Mtumba.
Dkt. Yonazi amehimiza Wakala hao wa majengo kuandaa mikakati endelevu ya kuimarisha na kuendelea kusimamia uendelezwaji wa Mji wa Serikali kuzingatia mahitaji ya sasa na baadae bila kuathiri utoaji wa huduma serikalini.



