DIB yawaalika wananchi kutembelea Nanenane, kupata elimu ya bima ya amana

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

BODI ya Bima ya Amana (DIB) imewataka wananchi kutumia fursa ya Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo ‘Nanenane’ kutembelea banda lake ili kujifunza kuhusu ulinzi wa amana zao na utaratibu wa fidia kwa fedha zinazowekwa katika benki na taasisi za fedha zenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania.

Akizungumza katika maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa DIB, Isack Kihwila, amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha wanaweka fedha zao katika benki na taasisi za fedha zilizosajiliwa na kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania ili kulindwa na mfumo wa bima ya amana.

Amesema kuwa fedha zinazowekwa katika taasisi zisizo rasmi haziwezi kufidiwa endapo taasisi hizo zitashindwa kutekeleza majukumu yake, hivyo akasisitiza umuhimu wa wananchi kupata elimu sahihi kuhusu huduma zinazotolewa na DIB.

Sambamba na hilo, Kihwila amewataka wenye amana wa iliyokuwa Benki ya FBME ambao bado hawajajitokeza kuchukua fedha zao kufanya hivyo haraka.

“Kuna kundi la wenye amana ambao bado hawajajitokeza kuchukua fedha zao licha ya fedha hizo kutengwa kwa ajili yao. Tunawasihi wafike ili kukamilisha taratibu za malipo,” amesema Kihwila.

Amefafanua kuwa baada ya kundi hilo kulipwa, DIB itaendelea na hatua ya kulipa asilimia 15 iliyobaki ya madai ili kuhakikisha kila mwenye amana anayestahili analipwa kwa asilimia 100 kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Aidha, amesema bado kuna baadhi ya wadai, wakiwemo wafanyakazi waliokuwa na madai yaliyofikishwa mahakamani, ambao malipo yao yanasubiri kukamilika kwa mchakato wa kuhakiki mali zilizobaki za benki hiyo.

Kihwila amesema DIB itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia Maonesho ya Nanenane kuhusu umuhimu wa bima ya amana na nafasi yake katika kulinda fedha za waweka amana pale taasisi za fedha zinaposhindwa kuendelea na shughuli zake.

spot_img

Latest articles

VETA yaleta suluhisho la kupiga mpunga kwa wakulima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na...

TAMKU yatanua uwekezaji, kujenga kiwanda cha korosho Tunduru

Na Mwandishi Wetu CHAMA Kikuu cha Ushirika cha TAMKU kimeanza kutekeleza mkakati wa kupanua...

TRA yasogeza huduma za kodi karibu na wananchi Nanenane

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imepeleka huduma zake katika Maonesho...

e-GA yaimarisha sekta ya kilimo kupitia mifumo ya kidijitali

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Serikali Mtandao (e-GA) imeeleza kuwa inaendelea kushirikiana na Wizara...

More like this

VETA yaleta suluhisho la kupiga mpunga kwa wakulima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na...

TAMKU yatanua uwekezaji, kujenga kiwanda cha korosho Tunduru

Na Mwandishi Wetu CHAMA Kikuu cha Ushirika cha TAMKU kimeanza kutekeleza mkakati wa kupanua...

TRA yasogeza huduma za kodi karibu na wananchi Nanenane

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imepeleka huduma zake katika Maonesho...