TRA yasogeza huduma za kodi karibu na wananchi Nanenane

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imepeleka huduma zake katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma ili kuwafikia wakulima, wafugaji, wafanyabiashara na wananchi wengine kwa kuwapatia elimu ya kodi pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Akizungumza katika maonesho hayo, mwakilishi wa TRA amesema banda la mamlaka hiyo linatoa huduma za usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), makadirio ya kodi kwa walipakodi wapya, pamoja na elimu kuhusu mifumo mbalimbali ya kidijitali inayotumiwa katika utoaji wa huduma za kodi.

Amesema pia wananchi wanaohitaji mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) wanapatiwa huduma kupitia mawakala waliopo bandarini, huku wafanyabiashara wakipata elimu kuhusu matumizi sahihi ya mashine hizo.

Aidha, TRA inaendelea kutoa elimu kuhusu Electronic Tax Stamp (ETS) kwa wazalishaji wa bidhaa hususan vinywaji na bidhaa nyingine zinazotakiwa kutumia stempu za kielektroniki, ili kuhakikisha uzingatiaji wa sheria za kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

Mbali na hilo, wananchi wanapatiwa elimu kuhusu misamaha na vivutio vya kodi vinavyopatikana katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, hatua inayolenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu fursa zilizopo kwa ajili ya kukuza uzalishaji.

Amewataka wananchi kutembelea banda la TRA lililopo ndani ya jengo la Taasisi za Fedha katika maonesho hayo, yanayoendelea kuanzia Agosti 1 hadi 8, ili kupata huduma na elimu mbalimbali za kodi.

Wakati huo huo, mmoja wa wananchi waliotembelea banda la TRA alisema alipata huduma ya usajili wa TIN kwa haraka baada ya awali kukumbana na changamoto za kimfumo wakati wa kufanya maombi.

Amesema alihudumiwa kwa muda mfupi na watumishi wa TRA, akieleza kuridhishwa na huduma aliyoipata na kuwataka wananchi wengine wenye mahitaji ya huduma za mamlaka hiyo kufika katika banda hilo ili kupata msaada kwa wakati.

spot_img

Latest articles

NIRC kutekeleza miradi 30 ya umwagiliaji, kufungua maelfu ya ajira kwa vijana

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imezindua mkakati wa...

TTB yampokea Mr. Alaya anayewania Guinness World Records

Na Mwandishi Wetu TANZANIA imepokea mhamasishaji amani duniani, Saddam Alaya (Mr. Alaya), ambaye anatekeleza...

VETA yaleta suluhisho la kupiga mpunga kwa wakulima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na...

TAMKU yatanua uwekezaji, kujenga kiwanda cha korosho Tunduru

Na Mwandishi Wetu CHAMA Kikuu cha Ushirika cha TAMKU kimeanza kutekeleza mkakati wa kupanua...

More like this