Katibu Mkuu Ahamasisha VETA Kutumia Sabasaba Kukuza Ujuzi na Fursa za Biashara

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) pamoja na taasisi nyingine za mafunzo ya ufundi kutumia Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kama jukwaa la kuonesha ubunifu, ujuzi na teknolojia zinazozalisha ajira na kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania.

Akizungumza baada ya kukagua maandalizi ya maonesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Balozi Salum alisema maandalizi yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 99 na kwamba Serikali inatarajia maonesho ya mwaka huu kuwa miongoni mwa yenye mafanikio makubwa.

Alisisitiza kuwa taasisi za mafunzo kama VETA zina nafasi muhimu ya kuandaa vijana wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda.

Alisema maonesho hayo yanapaswa kutumiwa si kwa ajili ya kuuza bidhaa pekee, bali pia kujenga ushirikiano wa kibiashara, kutafuta masoko mapya na kuonesha uwezo wa Watanzania katika ubunifu na uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vya kimataifa.

Aidha, Katibu Mkuu huyo alieleza kuridhishwa na ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini, hususan zile zinazotengenezwa na wajasiriamali wanawake, akisema zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa katika ubora na vifungashio na sasa zinaweza kushindana katika masoko ya kimataifa.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wazalishaji, wajasiriamali na taasisi za mafunzo ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania, kukuza ajira na kuimarisha mchango wa sekta ya viwanda katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

spot_img

Latest articles

YANGA YA KIHISTORIA! yatwaa ubingwa wa tano mfululizo

Na Mwandishi Wetu Wananchi Yanga wametwaa ubingwa wa tano mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania...

Msajili wa Hazina aonya taasisi za umma zenye utendaji duni Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeonya taasisi za umma zinazofanya vibaya kujitathmini na kuchukua hatua za...

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UZALISHAJI UMEME KITUO CHA JULIUS NYERERE

📌Yasema Kituo kinachangia asilimia 45 ya umeme katika Gridi ya Taifa 📌Yasisitiza ukamilishaji wa miradi...

MD TWANGE AFAFANUA CHANZO CHA HITILAFU ILIYOTOKEA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

📌 Aomba radhi kwa wateja wananchi na kuwahakikishia upatikanaji endelevu wa huduma ya umeme 📌...

More like this