Tanzania mwenyeji Miss World 2027, Serikali yajipanga kuandika historia mpya duniani

Na Winfrida Mtoi

TANZANIA imethibishwa rasmi kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa la urembo duniani ‘Miss World 2027’, huku Serikali ikisema imejipanga kuhakikisha linafanyika kwa mtindo wa pekee wa kuvutia ili kuandika historia duniani.

Mkataba wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo la 74, umesainiwa leo Aprili 20, 2026, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, mbele ya Waziri wa wizara hiyo, Paul Makonda, ambapo Tanzania itakuwa nchi ya pili Afrika kuandaa ya kwanza ilikuwa Afrika Kusini.

Hafla ya kusaini mkataba huo, imehudhuriwa na warembo mbalimbali akiongozwa na Miss World 2025, Opal Suchata, Miss World Africa 2025, Hasset Dereje, pamoja na Miss World Tanzania 2026, Latricia Ian, aliyepata taji hilo jana jijini Dar es Salaam.

Wengine ni wadau wadau wa sekta ya urembo nchini akiwamo mwaandaaji wa shindano Miss World Tanzania, Mustafa Hassanali, wanamitindo maarufu wa kimataifa wa Tanzania Millen Magessa ambaye ni Miss Tanzania 2001, Miriamu Odemba aliyewahi kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Earth 2008 na Jokate Mwegelo mshindi wa pili Miss Tanzania 2006.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Makonda amesema jukwaa la Miss World  linafuatiliwa na zaidi ya nchi 130, Tanzania ikitarajia kupata wageni wasiopungua 20,000. hivyo ili kulifanya kuwa bora zaidi Serikali itahusisha wadau mbalimbali katika maandalizi.

Ameeleza kuwa sherehe za mashindano hayo zitafanyika kwa siku 28, zikihusisha shughuli  tofauti tofauti kama vile ufunguzi, chakula cha wageni, mashindano ya vipaji, chakula cha hisani, maonesho ya mitindo pamoja na fainali kubwa ya Miss World.

“Kwa hiyo mwakani tuna mwezi mzima wa warembo.  Tanzania ipo tayari kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali kwa kuwa matukio yatakayofanyika katika kipindi hicho yatafungua fursa zaidi za kiuchumi,” amesema Makonda.

Aidha ameeleza kuwa  mpango wa Serikali ni  kuendelea kuomba  kufanya mashindano ya Miss World  kwa kipindi chote cha Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ikilenga  kuitangaza Tanzania kimataifa na kukuza Sekta za Utalii, Sanaa na Michezo.

Kwa upande wake Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Miss World, Julia Morley, aliitaja Tanzania kuwa ni sehemu yenye uzuri wa kipekee ambao bado haujajulikana kikamilifu duniani, akiahidi kusaidia ijulikane.

Julia ametoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya wadau wa habari  na serikali katika kuitangaza Tanzania kama kivutio kikuu cha utalii duniani, huku akisisitiza utunzani wa mazingira  ili rasilimali zilizopo zidumu.

“Kupitia mashindano ya urembo, washiriki  kutoka  nchi zaidi ya 140 watapata nafasi ya  kuifahamu Tanzania , jambo  ambalo litachochea utandawazi na umoja,” amesema.

spot_img

Latest articles

Latra yatangaza nauli mpya za mabasi, daladala

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa bei mpya za nauli kwa...

Serikali yatoa neno vipaji vya kuogelea Afrika Mashariki vikichanua Dar

Na Winfrida Mtoi ​MASHINDANO ya kuogelea kwa watoto ya ‘East Africa Development Swimming Gala’ yameanza...

Simba yapewa wakusanya kodi, Yanga maafande

Na Mwandishi Wetu DROO ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho,...

Waziri Mkuu ahimiza ufungaji kamera  viwanjani kudhibiti ushirikina

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba, amehimiza ufungaji wa kamera nyingi katika viwanja vya...

More like this

Latra yatangaza nauli mpya za mabasi, daladala

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa bei mpya za nauli kwa...

Serikali yatoa neno vipaji vya kuogelea Afrika Mashariki vikichanua Dar

Na Winfrida Mtoi ​MASHINDANO ya kuogelea kwa watoto ya ‘East Africa Development Swimming Gala’ yameanza...

Simba yapewa wakusanya kodi, Yanga maafande

Na Mwandishi Wetu DROO ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho,...