Na Mwandishi Wetu
NAHODHA msaidizi wa timu ya Yanga na mchezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Dickson Job, amefanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini leo Machi 11, 2026, kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Derby ya Kariakoo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe, amesema upasuaji huo umeenda vizuri na beki huyo anaendelea vizuri baada ya matibabu.
Job alipata jeraha hilo la goti katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba uliochezwa Machi Mosi, 2026 katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, uliomalizika kwa sare tasa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Klabu ya Yanga, beki huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili hadi mitatu akiendelea na matibabu kabla ya kurejea uwanjani.


