Na Mwandishi Wetu
KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa kosa la walinzi wake kugombana na kutoleana lugha za matusi wakati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo ulipigwa Machi 1,2026 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa mujibu wa kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi, Simba italazimika kulipa gharama za matengenezo ya mlango wa kuingilia chumba cha kufanyia mikutano ya wanahabari ambao walinzi wake walivunja ili kulazimisha timu hiyo kuingia kwa kutumia chumba hicho kwa ajili ya kuvalia kabla ya mchezo.
Pia mchezaji wa Simba David Kameta ametozwa faini y ash 1,000,000 kwa kosa la kuonekana akimwaga kimiminika kiwanjani dakika chache baada ya kuwasili uwanja wa Amaan kitendo kilichotafsiliwa kwa Imani za kishirikina.
Aidha Simba imetoza faini ya jumla ya sh 10, 000,000 kwa makosa ya kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi ambapo kila kosa imetozwa sh, 5, 000,000.


