‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu

MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili, umetajwa kuwa chachu mpya ya kuitangaza Tanzania kama kivutio cha utalii kupitia filamu, hususan Mlima Kilimanjaro, baada ya kuungwa mkono na ushirikiano kati ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Hatua hiyo ilibainishwa katika kikao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ambapo Katibu Mtendaji wa TFB, Dkt. Gervas Kasiga, amekutana na Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Ernest Mwamwaja, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Ephraim Balozi Mafuru, kwa lengo la kuimarisha matumizi ya filamu na michezo ya kuigiza kama nyenzo ya kimkakati ya kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.

Dkt. Kasiga amesema filamu zina nafasi kubwa ya kuonesha vivutio vya utalii, utamaduni na urithi wa Taifa, huku akibainisha kuwa ushirikiano huo utachochea ukuaji wa tasnia ya filamu sambamba na kuimarisha mwonekano wa Tanzania kimataifa.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu TFB, Emmanuel Ndumukwa, pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rams Film, Ram Ally, waandaaji wa mradi wa Guardians of the Peak, Shuyan Wang (Elizabeth Mrembo) Mratibu na Meneja Fidelis Ndyamkama.

Ushirikiano huo umeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za Serikali kutumia sanaa na filamu kama nyenzo ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake, ikiwemo kuhamasisha utalii, matumizi ya nishati safi na uelewa wa athari za mabadiliko ya tabia nchi kupitia maudhui ya filamu.

spot_img

Latest articles

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

Serikali yazindua Jukwaa la Vijana, yataja vijana kuwa mhimili Mkuu wa Maendeleo ya Taifa

Na Tatu Mohamed SERIKALI imezindua rasmi jukwaa la kitaifa la vijana lijulikanalo kama ‘Vijana...

Mradi wa Umeme Jua uko mbioni kukamilika- Salome Makamba

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema Mradi wa Umeme unaozalishwa...

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

More like this