Serikali yazindua Jukwaa la Vijana, yataja vijana kuwa mhimili Mkuu wa Maendeleo ya Taifa

Na Tatu Mohamed

SERIKALI imezindua rasmi jukwaa la kitaifa la vijana lijulikanalo kama ‘Vijana Platform’, likilenga kuwaunganisha vijana kutoka pande zote za nchi ili kushirikiana, kubadilishana mawazo na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Uzinduzi wa jukwaa hilo umefanyika leo Januari 10, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ukiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Nanauka amesema Serikali inatambua vijana kama mhimizaji mkuu wa nguvu kazi na maendeleo ya Taifa, kutokana na mchango wao mkubwa katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Ameeleza kuwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa takribani asilimia 77.3 ya Watanzania wote wana umri wa chini ya miaka 35, huku vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 wakichangia asilimia 34.4 ya idadi ya watu wote nchini.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Nguvu Kazi wa Taifa, Nanauka amesema vijana wanachangia asilimia 55.6 ya nguvu kazi yote ya Taifa, jambo linalothibitisha nafasi yao muhimu katika ujenzi wa uchumi na maendeleo endelevu ya Tanzania.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia majukwaa ya ushiriki, ajira, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha mchango wao unaimarishwa na kunufaisha Taifa kwa ujumla,” amesema Nanauka.

Amewataka vijana kutumia jukwaa la Vijana Platform kama chombo cha kujenga mitandao thabiti, kubadilishana mawazo ya maendeleo, kukuza ubunifu na vipaji, pamoja na kushiriki kikamilifu katika michakato ya kitaifa ikiwemo utungaji wa sera.

Nanauka ameongeza kuwa jukwaa hilo pia litalifungua Taifa katika ushirikiano wa kimataifa, kuwawezesha vijana wa Tanzania kujifunza kutoka kwa mataifa mengine na kushiriki katika programu za kimataifa zinazohusiana na maendeleo ya vijana.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwemo viongozi wa makundi ya vijana, wabunifu, wajasiriamali pamoja na wadau wa maendeleo.

Jukwaa hilo linatarajiwa kutoa fursa za mafunzo, warsha, programu za ushauri (mentorship), mijadala ya sera, pamoja na fursa za ushirikiano baina ya vijana na Serikali, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa.

spot_img

Latest articles

Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo...

Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Lifezone Metal

Na Mwandishi wa OMH Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amefanya mazungumzo na Bw. Keith Liddell,...

RC Chalamila akemea wimbi la utapeli na uporaji wa ardhi

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa muda wa...

Rais Samia kuzindua ujenzi wa matanki 15 ya mafuta Bandari ya Dar es Salaam

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa...

More like this

Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo...

Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Lifezone Metal

Na Mwandishi wa OMH Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amefanya mazungumzo na Bw. Keith Liddell,...

RC Chalamila akemea wimbi la utapeli na uporaji wa ardhi

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa muda wa...