Na Winfrida Mtoi
Mabao ya ugenini yameibeba Simba kwenda makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kutoka suluhu dhidi ya Nsingizini kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Simba imeingia makundi kutokana na ushindi wa mabao 3-0 ugenini katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo dhidi ya wapinzani wao hao ulifanyika nchini Eswatini.
Wanamsimbazi hao wanakamilisha idadi ya timu nne za Tanzania zilizoingia hatua ya makundi ya michuano ya CAF msimu huu ambapo Simba na Yanga Ligi ya Mabingwa wakati Azam FC na Singida BS zipo Kombe la Shirikisho Afrika.


