Heche akamatwa na Polisi Dar, apelekwa Tarime

Na Mwandishi Wetu

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Tanzania Bara, John Heche, amekamatwa na Polisi wakati akiingia Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda Tarime.

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amesema kiongozi huyo alikuwa anakwenda mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu inayoendelea.

Akizungumzia sababu za kukamatwa kwa Heche, mbeleza na waandishi wa habari leo Oktoba 22,2025, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Wakili Gaston Garubindi amesema wamefuatilia na kuambiwa na Jeshi la Polisi kuwa jambo la Heche   halipo Dar es Salaam lipo Tarime na wamedai kuwa  tayari wameshamsafirisha kuelekea huko.

“Taarifa ya Jeshi la Polisi wanadai ni kweli wamemkamata John Heche, kwa makossa ambayo hawajayasema, lakini anasema jambo lake lipo Tarime na kwamba  tuhuma zake zipo kule na tayari  wamemsafirisha kutoka Dar es Salaam kwenda Tarime.

“Kama Chama tunajipanga sasa kwa maana ya kuagiza mawakili waliopo Mkoa wa Mara na wengine kutoka Mwanza  ili  waelekee huko ili kutoa huduma ya Kisheria kwa Makamu Mwenyekiti,” amesema Wakili Garubindi.

Amesema Heche alikuwa hajapewa wito wowote wa kuitwa Polisi, hivyo wanasubiria atakapofikishwa hule watajua tuhuma zake ni nini.

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this