Na Mwandishi Wetu
Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa mara nyingine ikiifunga ikishinda bao 1-0 katika mchezo uliopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa wababe wa Dabi ya Karikoo ikiwafunga Simba mara ya sita mfululizo.

Mashabiki wa Simba wameonekana kuwa wangonye hasa baada ya Yanga kupata bao. Baada ya dakika 90 kumalizika licha mwamuzi kuongeza dakika 12, baadhi yao waliamua kuondoka.
