Simbu aweka rekodi ya pekee Tanzania, Rais Samia ampongeza

Na Mwandishi Wetu

Mwanariadha Alphonce Simbu ameweka rekodi ya kuwa mwanariadha wa kwanza Tanzania  kushinda medali ya dhahabu katika mbio za riadha za Dunia 2025 (World Athletics)  za kilomita 42 zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Japan mjini Tokyo.

Alphonce Simbu alivuka mstari wa kumalizia mbele ya Mjerumani Amanal Petros na kuibuka mshindi wa kwanza akifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu akimaliza kwa saa 2:09:4.

Medali hito ya Simbu ni ya kwanza kwa mwanariadha wa Tanzania kuwahi kushinda katika riadha.

“Nimeweka historia leo, ikiwa ni medali ya kwanza ya dhahabu ya Tanzania katika mashindano ya dunia. Nakumbuka mwaka 2017, kwenye mashindano ya dunia ya London, nilishinda shaba,” Simbu amesema baada ya ushindi wake.

Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha huyo, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamiii kwa kusema “Hongera sana Alphonce Simbu kwa Medali ya Dhahabu ya ushindi wa Mbio Ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo ndani ya saa 2:09:48 umeandika sehemu ya historia ya Taifa letu”

“Kama nilivyokusihi uliposhika nafasi ya pili kwenye Boston Marathon mwezi Aprili mwaka huu, ushindi wako ni matokeo ya nidhamu yako ya hali ya juu na kujituma kwa bidii kwenye kazi, umekuwa mfano bora kuhusu nguzo hizo mbili za kazi kwa wanariadha na wanamichezo wenzako na hata kwa wasiyo wanamichezo endelea kuipeperusha vyema na kuiheshimisha bendera ya Taifa letu” ameandika Dk. Samia.

spot_img

Latest articles

CAF yaipiga faini Simba, kucheza bila mashabiki

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba imepigwa faini ya Dola za Marekani 50,000 (...

ACT Wazalendo wakataa gari la INEC, Mpina atamba atashinda kwa asilimia 70

Na Winfrida Mtoi Chama Cha ACT Wazalendo kimegoma kupokea gari la Tume Huru ya Uchaguzi...

INEC yamteua Mpina kugombea Urais

Na Winfrida Mtoi TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imemteua rasmi  Luhaga Mpina kuwa...

More like this

CAF yaipiga faini Simba, kucheza bila mashabiki

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba imepigwa faini ya Dola za Marekani 50,000 (...

ACT Wazalendo wakataa gari la INEC, Mpina atamba atashinda kwa asilimia 70

Na Winfrida Mtoi Chama Cha ACT Wazalendo kimegoma kupokea gari la Tume Huru ya Uchaguzi...