Na Winfrida Mtoi
MASHABIKI wa timu ya Simba wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanashuhudia kilele cha Simba Day leo Septemba 10, 2025, burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na utambulisho rasmi wa kikosi chao cha msimu mpya wa 2025/2026.
Klabu ya Simba inahitimisha sherehe hizo kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaama baada ya wiki nzima kufanya shughuli mbalimbali za kijamiii katika maeneo mbalimbali nchini.
Wanamsimbazi hao waliotoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, hamu ya kubwa ni kuona wachezaji wao wapya waliosajiliwa wakati wa utambulisho na katika mchezo wa kirafiki na Gor Mahia ya Kenya utakaopigwa saa 11:00 jioni.



