Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ametangaza kuachana na majukumu hayo na kumteua Crescentius Magori kuchukua nafasi hiyo, huku CEO wa zamani wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez akiteuli miongoni mwa wajumbe wa Bodi hiyo.
Mo ametangaza mabadiliko hay oleo ambapo wajumbe wengine wakiwa ni Hussein Kitta, Azim Dewji, Rashidi Shangazi, Swedi Nkwabi, Zully Chandoo na George Ruhanga.
Amesema ameamua kuachana na majukumu hayo kutokana na muda mwingi kuwa mbali na klabu hivyo ameona umuhimu wa kupata viongozi waliopo karibu na wanaoweza kushiriki shughuli za kila siku.
