Polisi feki wakamatwa Pemba

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujifanya askari Polisi wa kitengo cha uchunguzi wa magari yaliyoibiwa.

Watuhumiwa hao ni Abdulkadir Uwiso (55) mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi na mkazi wa Buza na Khalfani Molo (60) mfanyabiashara wa Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi Mkoa Kaskazini Pemba, watu hao walifika katika Kijiji cha Konde na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ndogo ya Polisi Dar es Salaam, kitengo cha uchunguzi wa magari yaliyoibiwa.

Taarifa hiyo inasema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika Stendi ya Konde wakiwa tayari wamekamata gari moja ya abiria aina ya Coaster yenye namba za usajili Z510MY ambapo walimtaka dereva wa gari hiyo, Said Nassor Ali kituoni wakidai ni gari la wizi lililoibiwa Msumbiji.

Baada ya watuhumiwa kufanyiwa upekuzi walikutwa na redio call moja, funguo ya pingu na filimbi ya Jeshi la Polisi.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this