Waandishi wasisitizwa umakini kuelekea uchaguzi mkuu

Na Winfrida Mtoi

Wakati Tanzania ikiwa katika mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025,  waandishi wa habari wametakiwa kuwa makini na kuhakikisha wanasoma vizuri na kuelewa miongozo, kanuni ikiwamo Sheria ya  Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya waka 2024 pamoja na Sheria ya  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).

Rai hiyo imetolewa katika mafunzo ya siku moja, yaliyoandaliwa na Kampuni ya Media Brains kwa kushirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka Ujerumani, yakilenga kuwanoa wanahabari ili waelewe mbinu mbalimbali za kutekeleza majukumu yao wakati wa uchaguzi na kuepuka kuvunja sheria.

 Zaidi ya waandishi wa habari 30, wameshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika  hoteli ya Serene, jijini Dar es Salaam jana Agosti 15,2025  ikiwa ni muendelezo wa kutoa elimu ya uchaguzi kwa wahabari katika mikoa mbalimbali ya Tanzania hadi sasa tayari waandishi  katika mikoa saba wamepatiwa mafunzo hayo .

Katika mafunzo hayo, pamoja na kufundishwa sheria, wanahabari hao walipewa mbinu tofauti zitakazosaidia kufanya kazi kwa usahihi na kuepuka kujiingiza kwenye migogoro na kutoa nafasi sawa kwa wagombea bila kujali itikadi za vyama vyao au kuandika taarifa za uongo.

Akizungumza wakati wa akifundish, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu, amewataka wanahabari hao kuzingatia pia  kutoa taarifa zinazohusu usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko.

“Tafiti zinaonyesha kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, wagombea wanawake walipata nafasi ndogo kwenye vyombo vya habari ikilinganishwa na wanaume, hali inayohitaji kubadilika mwaka huu ili kujenga mfumo mzuri wa kidemokrasia. Vyombo vya habari vinapaswa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote bila kuonesha upendeleo,” amesema Kwayu.

Naye Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains, Absalom Kibanda, amesema kuelekea katika uchaguzi kuna mabadiliko ya sheria tatu umuhimu wanahabari wanatakiwa kuzifamu ambazo ni Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 (INEC), Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ambayo inatumika kwa mara ya kwanza mwaka huu na pia kuna mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2024.

“Kumekuwa na mabadiliko ya sheria kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ndiyo sababu sisi Media Brains imekwenda mbali kuwakumbusha wahabari si sheria pekee lakini pia kuhusu usalama na namna ya kuzungumza na wagombea bila kuegemea upande wowote. Pia kujilinda wenyewe na kupeleka habari sahihi kwa jamii ambayo ndiyo wapiga kura,” amesema Kibanda.

Aidha amesema kitu kingine cha kuzingatiwa na waandishi ni kufuata maadili ya uandishi wa habari.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains, Neville Meena, amesema endapo waandishi wa habari watazingatia mafunzo hayo wataweza kutekeleza majukumu yao kwa weledi na bila kupata matatizo.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...